TFF : UWANJA WA MKWAKWANI UMEFUNGULIWA KWA MICHEZO YA LIGI KUU



Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeiruhusu tena matumizi ya Uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga baada ya kufanyiwa marekebisho yaliyozingatia vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu.

Uwanja huo ulifungiwa awali kwa kushindwa kutimiza masharti ya leseni za klabu, lakini baada ya ukaguzi na marekebisho yaliyohitajika, sasa umebainika kukidhi vigezo vyote.

TFF imewahimiza wamiliki wa klabu na viwanja kuhakikisha miundombinu inatunzwa ili michezo ya Ligi Kuu iendelee kufanyika kwa kiwango bora na kuongeza ushindani.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post