MKOMBOZI JOGGING WATAMBULISHA WATATU WAPYA



Mkombozi Jogging Club ya Mbagala imetambulisha wanachama watatu wapya waliojiunga na Club hiyo 

Wanachama hao watatu ni Bebe Minah (ambaye alikuwa Afisa Habari Msaidizi Waugwana Jogging Club) pamoja na 
Chimamy Dida, Zasha Shaban ambao wote walikuwa wanachama Waugwana Jogging Club ya Mbagala Kizuiani.

Kupitia ukurasa rasmi wa Mkombozi Jogging waliandika "Wamefuata furaha"

Wakaongezea na Ujio wa mwanachama mwingine mpya ambaya wametumia "Dada anakuja kaa kwa kutulia"

Huu unakuwa ni usajili wa sita kwa Mkombozi Jogging Club ambapo utakumbuka mwishoni mwa mwaka mwezi Disemba 2025 walitambulisha wanachama watatu pia ambao ni Tatiana Og , Aisha Abou, Qween Momo ambao wote pia wametokea Waugwana Jogging Club.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post