HII HAPA IDADI YA VITI VILING'OLEWA KWA MKAPA



Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limesema Shabiki mmoja wa Timu ya CS SFAXIEN ya Tunisia ameumia katika fujo zilizotokea Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam huku jumla ya viti 256 ( 156 vya bluu 156 na Orange 100) viking’olewa na Mashabiki wa Club hiyo leo December 15, 2024 kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Simba SC na CS SFAXIEN.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Muliro Jumanne amesema fujo hizo zimesababishwa na Mashabiki wa Timu ya CS SFAXIEN kutoridhika na maamuzi ya Refa wa mchezo huo kuchezesha mechi hiyo kwa zaidi ya dakika saba ambazo aliziongeza kama dakika za nyongeza jambo lililopelekea timu ya Simba kupata goli la pili na la ushindi.

“Wachezaji wa ndani ya uwanja na “benchi” la fundi la timu ya CS SFAXIEN walikasirika, wakamfuata Muamuzi wa mchezo na kuanza kufanya vitendo vya kumshambulia, katika fujo hizo shabiki mmoja wa CS SFAXIEN aliumia na kupatiwa huduma ya kwanza na kuruhusiwa huku viti vya rangi ya blue 156 na Orange 100 viling’olewa na Mashabiki hao, Polisi itashirikiana na Mamlala nyingine za kisheria na soka kuona hatua za kuchukua dhidi ya vitendo hivyo ambavyo havikubaliki” - Kamanda Muliro.




Credit : Millard Ayo

 

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post