HAYA HAPA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI JESHI LA POLISI



Mkuu wa Jeshi la Polisi anawatangazia vijana walioomba ajira ya Jeshi la Polisi
kupitia mfumo wa Ajira (TANZANIA POLICE FORCE – RECRUITMENT
PORTAL) kuwa usaili utafanyika kuanzia tarehe 28/4/2025 saa 07:00 Asubuhi hadi tarehe 11/5/2025 kote nchini.

Kwa wasailiwa wenye elimu ya Shahada, Stashahada na Astashahada usaili
utafanyika jijini Dar es Salaam katika uwanja wa gwaride uliopo Kambi ya
Polisi (Police Barracks) barabara ya Kilwa nyuma ya kituo cha Polisi Kilwa
Road.

Kwa wasailiwa wenye elimu ya kidato cha Nne na cha Sita usaili utafanyika
kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa waliyoichagua wakati wa kutuma
maombi.



Orodha ya waliochaguliwa kufanya usaili imeambatishwa kwenye PDF hapa chini:



 

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post