Dovya Jogging Sports Club imetangaza rasmi kufanyika kwa bonanza lao maalum lililopewa jina la “ASANTE JOGGING”, litakalofanyika tarehe 07 Juni 2026 katika uwanja ambao utatangazwa baadaye.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Club hiyo, Iddy Mbelwa, amesema Bonanza hilo linalenga kutoa shukrani kwa mchango mkubwa uliotolewa na wanajogging mbalimbali katika kuendeleza na kukuza mchezo wa jogging.
Mbelwa ameongeza kuwa bonanza hilo litakuwa jukwaa maalum kwa watu binafsi au vikundi vyote vinavyotamani kutoa shukrani zao, iwe ni kwa maneno au kwa njia ya zawadi.
“Kwa yeyote atakayehitaji kutoa shukrani, iwe kwa maneno au zawadi ya aina yoyote, jukwaa linawasubiri,” amesema Mbelwa.
Bonanza la ASANTE JOGGING linatarajiwa kuwa tukio la kipekee litakalokusanya wanajogging na wadau mbalimbali kwa lengo la kusherehekea mafanikio na kuthamini mchango wa kila mmoja katika safari ya mchezo huo.


Post a Comment