TEJA KUFANYA UCHAGUZI MKUU FEBRUARI 22, 2026



Chama cha Jogging Wilaya ya Temeke (TEJA) kimetangaza rasmi kufanya Uchaguzi Mkuu tarehe 22 Februari 2026, katika Ukumbi wa Iddi Nyundo, Manispaa ya Temeke, kuanzia saa 3:00 asubuhi.

Nafasi zitakazowaniwa katika Uchaguzi huo ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina na Wajumbe 10 wa Kamati Tendaji, ambapo nafasi mbili ni maalum kwa wanawake.

Fomu za kuwania nafasi zitapatikana katika ofisi za TEJA kuanzia 21 Januari hadi 01 Februari 2026. 

Kamati ya Uchaguzi, inayoongozwa na Mwenyekiti, Mzee Hassan Mbaya imewahimiza wanachama wote wenye sifa na nia ya uongozi kujitokeza mapema.

TEJA imeahidi uchaguzi huru, wa haki na wa uwazi, na imewataka wanachama wote kushiriki katika mchakato huo.







0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post