RAIS WA SENEGAL AWAZAWADIA WACHEZAJI MILIONI 300 NA VIWANJA BAADA YA UBINGWA WA AFCON





Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, ametangaza zawadi nono kwa wachezaji na benchi la ufundi la timu ya taifa kufuatia ushindi wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini humo, kila mchezaji wa timu ya taifa ya Senegal atapatiwa zawadi ya fedha taslimu kiasi cha Euro 115,000 (takribani Shilingi milioni 339 za Tanzania), pamoja na kiwanja cha mita za mraba 1,500 kwa ajili ya ujenzi wa makazi katika mji mkuu, Dakar.




Aidha, kila mjumbe wa Shirikisho la Soka la Senegal atapewa Euro 75,000 (takribani Shilingi milioni 217) pamoja na kiwanja cha kujenga nyumba, ikiwa ni sehemu ya kuthamini mchango wao katika mafanikio ya timu hiyo.

Kwa upande mwingine, jumla ya Euro 465,000 (takribani Shilingi bilioni 1.36) itagawiwa kwa maofisa kutoka Wizara ya Michezo walioisindikiza timu ya taifa katika mashindano hayo.



Senegal ilitwaa ubingwa wa AFCON baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Morocco katika mchezo wa fainali.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post