STEVEN MUKWALA AONDOKA SIMBA, ATUA LIBYA



Klabu ya Al Nasser ya nchini Libya imemtambulisha rasmi mshambuliaji wa Simba SC, Steven Mukwala, kuwa mchezaji wao mpya katika dirisha dogo la usajili.

Kupitia ukurasa wao rasmi wa Instagram, Al Nasser wametangaza kukamilika kwa dili hilo, wakimkaribisha Mukwala kujiunga na kikosi chao kwa lengo la kuimarisha safu ya ushambuliaji.

Mukwala, ambaye ni raia wa Uganda, amekuwa miongoni mwa washambuliaji waliokuwa wakitegemewa na Simba SC katika mashindano ya ndani na ya kimataifa, akionesha uwezo mkubwa wa kufunga na kushambulia kwa nguvu.




Hatua ya Mukwala kujiunga na Al Nasser inatajwa kuwa sehemu ya mkakati wa klabu hiyo kuongeza ushindani ndani ya ligi ya Libya, huku mashabiki wakingoja kuona mchango wake katika kikosi hicho kipya.

Simba SC bado haijatoa taarifa rasmi kuhusu uhamisho huo.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post