SENEGAL YATANGAZA MAPUMZIKO YA KITAIFA KUSHEREHEKEA UBINGWA WA AFCON




Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, ametangaza kuwa leo Jumatatu ni siku ya mapumziko ya Kitaifa nchini humo, kufuatia Timu ya Taifa ya Senegal kutwaa ubingwa wa AFCON.

Mapumziko hayo ni kama sehemu ya kuadhimisha ushindi huo wa kihistoria, uliowaunganisha wananchi wa Senegal katika shangwe na furaha kubwa baada ya timu yao kuibuka mabingwa wa soka barani Afrika.

Hatua hiyo imepokelewa kwa furaha na wananchi wengi, ikionyesha namna serikali inavyothamini mchango wa michezo, hususan soka, katika kuimarisha umoja wa kitaifa na kuleta fahari kwa taifa.



Ubingwa huo wa AFCON 2025 umeiweka Senegal katika historia ya soka la Afrika, huku sherehe mbalimbali zikitarajiwa kufanyika nchini kote kuadhimisha mafanikio hayo makubwa.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post