KOCHA WA SENEGAL AOMBA RADHI




Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Senegal, Pape Thiaw, ametoa kauli ya kujitathmini na kuomba radhi baada ya kuagiza wachezaji wake kuondoka uwanjani kama ishara ya kupinga maamuzi ya refarii katika fainali ya AFCON.

Thiaw alisema kuwa hakuridhishwa na uamuzi wake wa awali wa kuwaamuru wachezaji kuondoka uwanjani, na alieleza kujutia matendo hayo.

“Sikuridhishwa kabisa kwamba niliwaambia wachezaji wangu waondoke uwanjani. Naomba radhi” alisema 

Kocha huyo aliongeza kuwa baada ya kutafakari, aliwaamuru wachezaji wake warudi uwanjani, akifafanua kuwa mara nyingine majibu ya hisia za ghafla yanaweza kuathiri uamuzi.

“Baada ya kutafakari, niliwapa maagizo ya kurudi. Wakati mwingine unaweza kuchukua maamuzi hasira. Lakini tunakubali makosa ya refarii.” alisema Pape Thiaw

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post