SIMBA NA MTIBWA SUGAR WAGAWANA ALAMA MEJA JENERALI ISAMUHOYO



Simba SC imelazimika kugawana alama na Mtibwa Sugar baada ya sare ya bao 1-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliochezwa katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo.


Simba SC ilianza vyema mchezo huo kwa kupata bao la kuongoza dakika ya 19 kupitia kwa mshambuliaji Elie Mpanzu, bao lililowapa ujasiri wekundu wa Msimbazi kudhibiti sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza.


Hata hivyo, Mtibwa Sugar ilirejea kwa nguvu kipindi cha pili na kufanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 60 kupitia kwa Fredrick Magata.



Licha ya jitihada za pande zote mbili kutafuta bao la ushindi katika dakika zilizobaki, hakuna timu iliyoweza kuongeza bao, na hivyo mchezo kumalizika kwa sare ya 1-1.


Matokeo hayo yameifanya kila timu kuondoka na pointi moja, Simba wakifikisha alama 13 nafasi ya 4 katika msimamo wa Ligi huku Mtibwa Sugar wao wakifikisha alama 11 nafasi ya 8 katika msimamo wa Ligi.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post