MATOKEO YA MECHI ZA LIGI KUU YA WANAWAKE




Mzunguko wa 9 wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) msimu wa 2025/2026 umechezwa leo Januari 18, 2026 katika viwanja mbalimbali nchini, ukishuhudia michezo yenye ushindani mkubwa na matokeo muhimu kwa kila timu.

Tausi FC iliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Geita Queens katika mchezo uliopigwa Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam. Ushindi huo uliipa Tausi FC alama tatu muhimu nyumbani.

Alliance Girls waliendelea kuonyesha uimara wao baada ya kuifunga Ruangwa Queens mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa Majaliwa, Lindi, huku Ceasiaa Queens wakicharaza Bilo FC mabao 3-0 katika Uwanja wa Nyamagana, Mwanza.



Simba Queens walipata ushindi wa ugenini baada ya kuilaza Mashujaa Queens mabao 2-1 katika Uwanja wa Kituo cha Ufundi cha TFF, Kigamboni, matokeo yaliyoimarisha nafasi yao katika msimamo wa ligi.

Katika michezo mingine, Fountain Gate Princess waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Bunda Queens mkoani Manyara, huku Yanga Princess wakifanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Queens katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post