Mchambuzi wa soka, Geoff Lea, amesema kuwa Simba SC bado ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu, akisisitiza kuwa ni mapema sana kuhitimisha hatma ya timu hiyo baada ya michezo michache ya mwanzo.
Akizungumzia mwenendo wa ligi, Geoff Lea amesema hakuna bingwa anayepatikana ndani ya mechi sita pekee, akibainisha kuwa ligi ina jumla ya michezo 30 na Simba SC ndiyo kwanza imecheza mechi sita tu.
“Hakuna bingwa wa mechi sita. Simba SC bado ina uwezo mkubwa wa kutwaa ubingwa msimu huu. Ligi ina mechi 30, na Simba wamecheza mechi chache sana,” amesema Geoff Lea.
Ameongeza kuwa hata kama kutakuwa na changamoto za ndani au Simba SC ikajikuta iko nyuma kwa tofauti ya alama tatu dhidi ya timu kinara, bado hilo si jambo la kuamua hatima ya ubingwa.
“Kama kuna mgogoro ndani ya Simba SC na wakazidiwa alama tatu na kinara, je mgogoro huo ukimalizika nini kinaweza kutokea? Kila kitu bado kiko wazi,” ameongeza.
Kauli ya Geoff Lea imekuja wakati kukiwa na mijadala miongoni mwa mashabiki kuhusu mwenendo wa Simba SC mwanzoni mwa msimu.

Post a Comment