ETO’O AMPONGEZA SADIO MANÉ "NINAMPA HESHIMA YA KIPEKEE"



Rais wa Shirikisho la Soka Cameroon na gwiji wa soka barani Afrika, Samuel Eto’o, amempongeza nahodha wa Senegal, Sadio Mané, kwa mchango wake mkubwa ndani na nje ya uwanja katika michuano ya AFCON.

Eto’o amesema kuwa Mané hakuchangia tu ushindi wa taji hilo, bali pia aliokoa taswira ya timu ya taifa ya Senegal wakati wa tukio la sintofahamu lililotokea katika fainali, ambapo wachezaji waliondoka uwanjani kupinga uamuzi wa mwamuzi.

“Sadio Mané hakusaidia tu kushinda mashindano, bali pia aliokoa heshima ya timu ya taifa. Kuondoka uwanjani kungekuwa na madhara makubwa sana kwa Senegal,” amesema Eto’o.

Gwiji huyo ameongeza kuwa kitendo cha Mané kuwashawishi wachezaji wenzake kurejea uwanjani kinaonesha uongozi wa hali ya juu, maadili bora na ukomavu wa kipekee.

“Sadio ni mmoja wa mashujaa wakubwa wa bara letu. Ninampa heshima ya kipekee kwa maadili na uongozi wake. Ninajivunia kumuita rafiki yangu, na mchango wake katika kuwaongoza wenzake hadi ushindi ulikuwa wa kipekee,” ameongeza Eto’o.

Eto’o pia ameeleza matumaini yake kuwa Mané atatwaa tena tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika, akisisitiza kuwa mwenendo wake, hasa katika fainali hiyo, ni mfano halisi wa kiongozi wa kweli.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post