Kipa wa timu ya taifa ya Senegal, Édouard Mendy, amekanusha vikali madai yanayodai kuwa Brahim Diaz alikosa penalti kwa makusudi katika fainali ya AFCON dhidi ya Senegal.
Akizungumza baada ya mchezo huo, Mendy amesema hakuna uwezekano wowote wa mchezaji kukosa penalti kwa makusudi katika mazingira ya ushindani mkubwa kama yale ya fainali.
“Hapana, kabisa si kweli. Tunapaswa kuwa makini na maneno yetu. Unadhani kweli dakika moja imebaki, taifa limekaa miaka 50 likisubiri taji, halafu tukakubaliana jambo kama hilo?” amesema Mendy.
Kipa huyo amesisitiza kuwa Diaz alikuwa na dhamira ya kufunga, lakini yeye kama kipa alitimiza wajibu wake.
“Alitaka kufunga, na mimi ninastahili pongezi kwa kuokoa penalti hiyo, hakuna zaidi ya hapo,” ameongeza.
Kauli ya Mendy imekuja kufuatia mijadala katika mitandaoni kuhusu namna penalti hiyo ilivyopigwa na kuokolewa.
Hata hivyo, Mendy ameweka wazi kuwa tukio hilo lilikuwa sehemu ya kawaida ya ushindani wa soka, na ushindi wa Senegal ulitokana na juhudi halali uwanjani.

Post a Comment