Senegal imetwaa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Morocco, katika fainali iliyochezwa kwa ushindani mkubwa.
Mchezo huo ulilazimika kwenda dakika 120, kufuatia dakika 90 za kawaida kumalizika kwa sare tasa (0-0).
Bao la ushindi kwa Senegal lilifungwa na Pape Gueye na kuwapa ushindi wa kihistoria dhidi ya Morocco mbele ya mashabiki wao.
Senegal wamehitimisha michuano hiyo wakiwa mabingwa wa Afrika, wakithibitisha nafasi yao kama moja ya mataifa yenye nguvu zaidi katika soka la bara la Afrika.


Post a Comment