SIMBA YAANZA SAFARI YA CAFCL TUNISIA, CHAMA NDANI YA KIKOSI




Kikosi cha Simba SC kimeanza safari alfajiri ya leo, Januari 21, 2026, kuelekea nchini Tunisia kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya Esperance de Tunis.

Katika kikosi hicho amejumuishwa pia kiungo mshambuliaji, Clatous Chama, ambaye alitambulishwa rasmi jana kama mchezaji wa Simba SC. 



Simba SC itashuka dimbani siku ya Jumamosi, Januari 24, 2026, ugenini nchini Tunisia, kuivaa Esperance de Tunis katika mchezo wa Kundi D wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezo huo ni muhimu kwa Simba katika mbio za kusaka nafasi ya kusonga mbele kwenye hatua inayofuata ya mashindano hayo ya ngazi ya juu barani Afrika.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post