Shirikisho la Kandanda la Morocco (FRMF) limetangaza rasmi kuwa litachukua hatua za kisheria kupitia Shirikisho la Kandanda Barani Afrika (CAF) na Shirikisho la Kandanda Duniani (FIFA), kufuatia kitendo cha timu ya taifa ya Senegal kuondoka uwanjani wakati wa fainali ya AFCON dhidi ya Morocco.
Kwa mujibu wa taarifa ya FRMF, hatua hiyo ya Senegal ilichukuliwa baada ya Morocco kupewa penati, uamuzi ambao umeelezwa kuthibitishwa kuwa sahihi na wataalamu wa sheria za mpira wa miguu.
Morocco imesisitiza kuwa tukio hilo lilivuruga mtiririko wa kawaida wa mchezo na kuathiri hali ya kisaikolojia na utendaji wa wachezaji.
Shirikisho hilo limesema suala hilo linapaswa kushughulikiwa kupitia njia rasmi za kisheria ili kulinda heshima, haki na uadilifu wa soka la Afrika.
Morocco imesisitiza kuwa matukio kama hayo hayapaswi kupewa nafasi katika mashindano makubwa ya kimataifa na kwamba hatua za kinidhamu zichukuliwe kwa mujibu wa kanuni za CAF na FIFA.


Post a Comment