KOCHA WA SENEGAL ASIMAMISHWA KWA MUDA NA CAF



Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) limetangaza kumsimamisha kwa muda usiojulikana kocha mkuu wa timu ya taifa ya Senegal, Pape Thiaw, kufuatia tukio la kuhamasisha wachezaji wake kuondoka uwanjani wakati wa mechi ya fainali ya AFCON.

Tukio hilo lilitokea dakika za mwisho za mchezo baada ya mwamuzi kuipa Morocco mkwaju wa penalti uliokuwa na utata, uamuzi uliosababisha hisia kali miongoni mwa wachezaji wa Senegal pamoja na benchi la ufundi.




Kwa kuonyesha kutoridhishwa na maamuzi ya waamuzi, Thiaw aliwaamuru wachezaji wake kuondoka uwanjani, hali iliyosababisha mchezo kusitishwa kwa takribani dakika 20.

CAF imesema kuwa kitendo hicho ni ukiukwaji wa kanuni za mechi na kinadhalilisha heshima na misingi ya mashindano ya AFCON. Kutokana na hilo, shirikisho hilo limechukua hatua ya kinidhamu kwa kumsimamisha kocha huyo wakati uchunguzi zaidi ukiendelea.

Uamuzi huu unakuja licha ya Senegal kuibuka mabingwa wa AFCON 2025, huku CAF ikisisitiza kuwa ushindi hauhalalishi vitendo vinavyokiuka nidhamu, na kwamba viongozi wa timu wanapaswa kuonyesha busara, heshima na mfano bora

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post