Beki wa klabu ya Liverpool, Ibrahima Konaté, ametangaza kwa huzuni kifo cha baba yake, Hamady Konaté, kupitia ukurasa wake wa Instagram Story.
Taarifa hiyo imegusa mioyo ya mashabiki wengi wa soka duniani, ambao wameendelea kumfariji na kumpa pole mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa.
Katika kumbukumbu za awali, Konaté aliwahi kusimulia hadithi yenye kugusa hisia kuhusu ushauri alioupata kutoka kwa baba yake alipokuwa akianza safari yake ya soka la kulipwa.
“Nilipoondoka kwenda (kujiunga na Clubu) Sochaux nikiwa na umri wa miaka 15, baba yangu aliniambia jambo moja tu: ‘Kuwa mtu mwema.’
"Miaka mitatu baadaye, nilipoondoka (katika) akademi, nilipokea ujumbe kutoka kwa (mmoja ya) wasimamizi aliyeitwa Farid aliandika ujumbe uliosomeka ‘Ibra, asante. Nimefanya kazi hii kwa miaka ishirini, sijawahi kumuona mtu kama wewe. Nakutakia kila la heri katika maisha yako ya baadaye ya soka.’
Ujumbe huo niuhifadhi, kwa sababu nilijua kuwa nilikuwa nimetimiza jukumu alilonipa baba yangu" alisema Ibrahim.
Maneno haya yanaonyesha namna marehemu Hamady Konaté alivyokuwa msingi mkubwa wa maadili, nidhamu na mafanikio ya mwanawe, si tu kama mchezaji bora, bali pia kama binadamu mwenye heshima.

Post a Comment