EDIN DŽEKO AJIUNGA NA KLABU YA SCHALKE O4




Mshambuliaji mkongwe Edin Džeko amekamilisha rasmi uhamisho wake kutoka Fiorentina kwenda klabu ya Schalke 04, inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Ujerumani (2. Bundesliga).

Džeko (39) amejiunga na Schalke kwa uhamisho wa bure, huku mkataba wake ukijumuisha bonasi kulingana na kiwango cha uchezaji.

Nyota huyo anarejea tena Ujerumani, ambako aliwahi kung’ara akiwa na klabu ya Wolfsburg na kusaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa Bundesliga mwaka 2009, hatua iliyomfungulia milango ya kucheza katika klabu kubwa barani Ulaya.

Katika safari yake ya soka, Džeko amewahi kuzichezea klabu kadhaa maarufu zikiwemo Manchester City, AS Roma, Inter Milan, Fenerbahçe, Fiorentina, na sasa Schalke 04.

Akiwa na uzoefu, uwezo wa kufunga, anatarajiwa kuwa nguzo muhimu ndani ya klabu ya Schalke 04 katika harakati zao za kurejea Bundesliga.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post