AZAM FC YAICHAPA COASTAL UNION 3-0



Klabu ya Azam FC imeendelea kuonesha ubora wake katika Ligi Kuu ya NBC baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union, katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Azam FC walianza kwa kasi na kufungua ukurasa wa mabao mapema dakika ya 24, kupitia Yahya Zayd aliyefunga kwa mkwaju wa penalti, baada ya Coastal Union kufanya kosa ndani ya eneo la hatari.

Dakika ya 35, kiungo nyota Feisal Salum aliiongezea Azam FC bao la pili kwa shuti kali lililoshindwa kudhibitiwa na mlinda mlango wa Coastal Union, na kuiweka timu yake katika nafasi nzuri kabla ya mapumziko.




Kabla ya filimbi ya mwisho ya kipindi cha kwanza dakika ya 45+2', Jephte Kitambala alihitimisha karamu ya mabao kwa kufunga bao la tatu na kuifanya Azam FC kwenda mapumzikoni ikiwa mbele kwa mabao matatu.

Katika kipindi cha pili, Azam FC iliendelea kutawala mchezo kwa umakini, huku Coastal Union ikishindwa kupata bao la kufutia machozi, na hivyo mchezo kumalizika kwa ushindi wa mabao 3-0 kwa Azam FC.


Ushindi huo umeifanya Azam FC kuendelea kukusanya alama tatu muhimu nyumbani, katika mbio za kujiimarisha kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post