MO DEWJI ATOA TAMKO HILI KUHUSU UAMUZI WA CAF



Rais wa Klabu ya Simba SC na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohammed Dewji, ameandika barua ya wazi kwa mashabiki wa klabu hiyo akieleza masikitiko yake juu ya uamuzi wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kuhamishia fainali ya Kombe la Shirikisho huko Zanzibar, badala ya kufanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kama ilivyotarajiwa.


Katika tamko hilo, Dewji ameeleza kuwa Simba SC, kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali, walitekeleza kila hitaji lililotolewa na CAF kuhusu ukarabati na maandalizi ya uwanja huo. Hata hivyo, licha ya juhudi hizo, CAF imeendeleza uamuzi wake wa kuhamisha mechi hiyo.


“Kwa mtazamo wangu wa kibinafsi, hatukutendewa haki,” amesema Dewji, akionyesha wazi kutoridhishwa na uamuzi huo ambao amesema umeathiri si tu Simba SC bali pia mashabiki na wadau wote waliokuwa wakijiandaa kushuhudia tukio hilo la kihistoria.


Pamoja na masikitiko hayo, Dewji amesema klabu hiyo haijakata tamaa, na itaelekea Zanzibar kwa mshikamano na dhamira ya kutimiza wajibu wake, akiwataka wachezaji kuingia uwanjani kwa ujasiri na mashabiki kugeuza hasira zao kuwa nguvu ya kushangilia.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post