Temeke Jogging Sports Club imewatangazia umma na Wanatasnia wa mchezo wa Jogging nchi nzima kuwa kuanzia leo tarehe 23/03/2025, haitoshirikiana kwa namna yoyote na ndugu VAN KEMPES mmiliki wa ukurasa wa Club Tz katika kazi za klabu hiyo hususani swala la kurusha hewani maudhui yanayohusiana na bonanza lao linalotarajia kufanyika tarehe 01/06/2025.
"Tumechukua uamuzi huu baada ya kufanya uchunguzi wa kadhia inayomhusu ndugu VAN KEMPES ambayo kimsingi inatia doa tasnia yetu ya mchezo wa jogging.
"Baada ya kujiridhisha kupitia vyanzo vyetu vya taarifa tunawatangazia kazi na ndugu VAN KEMPES ili umma kuwa kuanzia sasa hatufanyi kazi na kulinda hadhi na heshima ya Klabu yetu na mchezo wa Jogging kwa ujumla" ilisema sehemu ya Taarifa ya Temeke Jogging Sports Club.
Pia, Temeke Jogging Sports Club wameomba radhi kwa Chama cha mbio za pole Wilaya ya Temeke (TEJA).
"Tunaomba radhi kwa wanachama wetu, wanatasnia kwa ujumla na Chama cha mbio za pole Wilaya ya Temeke (TEJA) kwa yote yaliyotokea".
Utakumbuka hivi karibuni Temeke Jogging Sports Club walimtangaza Van Kempes kuwa balozi wao na walisafiri nae kwenda mkoani Mbeya katika kile walichokiitwa #MbeyaTour ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea katika Bonanza lao.
Pia taarifa hii inakuja ikiwa ni siku chache tu zimepiga kufungiwa na Chama cha mbio mbio za pole wilaya ya Ilala maarufu kama IJA kwa kile walichodai ni utovu wa nidhamu.



Post a Comment