WAZIRI MKUU AAGIZA NIFFER AKAMATWE





Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kumkamata mfanyabiashara maarufu nchini Niffer kutokana na kile kilichoelezwa kuwa kuchangisha michango ya maafa ya Kariakoo kinyume na taratibu


Majaliwa ametoa maagizo hayo leo, Jumatatu Novemba 18, 2024 baada ya kufanya ukaguzi wa hatua iliyofikiwa kwenye zoezi la uokoaji linaloendelea kwenye jengo la ghorofa lililoporomoka kwenye soko la kimataifa la Kariakoo, jijini Dar es Salaam


Majaliwa amesema Niffer amekuwa akitumia mitandao yake ya kijamii kuchangisha michango kinyume na taratibu, hivyo kuagiza Jeshi la Polisi limkamate mfanyabiashara huyo na kisha kumuhoji ni wapi amepata kibali cha kuchangisha fedha hizo


Sambamba na hilo ameagiza account zake alizokuwa anatumia kuendesha makusanyo hayo zote zifungwe haraka iwezekanavyo, katika hilo Majaliwa amesema amemsikia Niffer akisema amekusanya milioni 30+ na kwamba anasema amenunua maziwa kwa ajili ya Kariakoo jambo ambalo pia ametaka ahojiwe


Baada ya kutoa agizo hilo, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila alimueleza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwa mtu huyo tayari ameshakamatwa.


Katika hatua nyingine, Majaliwa ameagiza mmiliki wa jengo la ghorofa Kariakoo lililoporomoka na kuleta maafa atafutwe na vyombo vya dola haraka iwezekanavyo.


 

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post