CEDRIC KAZE HUYO AFRIKA KUSINI, NABI ASEMA HILI

 




Kulingana na taarifa kutoka nchini Afrika Kusini zinasema kuwa, aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Nabi katika klabu ya Young Africans, Cedric Kaze, ndiye anayepewa nafasi kubwa ya kuchukua nafasi ya Da Cruz kama kocha msaidizi ndani ya timu ya Kaizer Chiefs.



Kaizer Chiefs wanajikuta wakisaka kocha msaidizi mpya baada ya kuondoka kwa Fernando Da Cruz mwezi Agosti amabaye ametimkia ndani ya shirikisho la soka la Morocco.


Da Cruz amejiunga na shirikisho la soka la Morocco kama Mkurugenzi wa Ufundi.



Akithibitisha habari hizo, Nabi pia alidokeza uwezekano wa kutafuta mbadala wake huku Cedric Kaze akiwa ndiye anayelengwa zaidi.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post