Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Sc, Ahmed Ally ametoa sababu tatu za klabu yao kupata ushindi katika mchezo wa Oktoba 19 dhidi ya watani zao Yanga.
Kupitia katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, Ahmed amesema wamejipanga vizuri kupata ushindi katika mchezo huo ili kurejesha heshima ya Simba ambayo ilipotea msimu uliopita kwa kufungwa mechi zote mbili (raundi ya kwanza na ya pili).
"Tumejiandaa vizuri na tumejianda kinyama zaidi ili kupata ushindi siku ya tarehe 19 kwa sababu tatu
SABABU YA KWANZA, Kurejesha heshima yetu sisi kama Simba SC sababu hata tukizifunga timu zote duniani sio kitu kama tutashindwa kuifunga yanga Sc maana yake tutakosa heshima kwenye utawala wetu
SABABU YA PILI, tunahitaji kupata ushindi kwenye mchezo huo ili kukusanya alama tatu sababu tupo kwenye mbio za ubingwa na ili kupata ubingwa lazima kujiahakikishie kupata alama tatu kwa mpinzani ambaye unashindana nae kupata ubingwa
SABABU YA TATU, tunataka kufuta historia inayotaka kutengenezeka kwamba wao wanatumudu au wanatuweza, na kutuzoea tunataka wawe na uoga wanapojua wanakutana na Simba

Post a Comment