Yanga Princess yapigwa nje ndani na Simba Queens

 


Timu ya Yanga Princess imepokea kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Simba Queens katika mchezo wa raundi ya pili ya Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara uliopigwa katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Simba walianza kupata bao la kwanza kupitia kwa Aisha Mnuka dakika ya 49' baadae dakika ya 66' nyota wa kimataifa wa Kenya, Jentrix Shikangwa akaindikia Simba Queens bao la pili.


Dakika ya 90'+2 Aisha Mnuka akafunga bao lake la pili na la tatu kwa Simba Queens na dakika cheche kabla ya mchezo kumalizika Kaeda Wilson akaifungia  Yanga Princess bao dakiki ya  90'+5.

Yanga Princess wamepigwa nje ndani msimu huu, utakumbuka katika mchezo wa kwanza walipigwa 3-1 na leo katika mchezo wa raundi ya pili pia wamekubali kipigo cha 3-1. 







0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post