Azam FC yaifuata Simba SC fainali Kombe la Muungano



Azam FC imetinga fainali ya kombe la Muungano 2024 kufuatia ushindi wa 5-2 dhidi ya KMKM FC kwenye Nusu Fainali ya pili michuano hiyo inayoendelea kutimua vumbia visiwani Zanzibar.


Mabao ya Azam FC katika mchezo huo yamefungwa na Abdul Sopu aliyefunga mabao mawili dakika ya 7' na dakika ya 42', beki wa kulia, Nathaniel Chilambo dakika ya 9', winga Idd Seleman 'Nado' dakika ya 49' pamoja na  nyota toka timu ya vijana ya Azam FC, Kishindo dakika ya 74' huku mabao ya KMKM FC yote mawili yakifungwa na Abdurahman Alli




Azam FC watachuana na Simba Sc kkatika mchezo wa fainali utakaopigwa siku ya Jumamosi Aprili 27, 2024 katika uwanja wa New Amaan Complex, Saa 2:15 Usiku.


 

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post