USM Alger Wagoma Kuingiza Timu Uwanjani Katika Mchezo wa Nusu Fainali CAFCC



Mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho baranin Afrika kati ya RS Berkane ya Morocco dhidi ya USM Alger ya Algeria umeshindwa kufanyika baada ya klabu ya USM Alger kugoma kuingia uwanjani.




Utakumbuka wiki iliyopita Shirikisho la soka Afrika (CAF) liliwapa ushindi wa mabao 3-0 klabu ya RS Berkane dhidi ya USM Alger ya Algeria kwenye mchezo ambao ulitakiwa kuchezwa Algeria lakini haukufanyika.




Sababu ya Berkane kupewa mabao 3-0 bila kucheza ni kwamba Mamlaka za soka nchini Algeria na serikali yao zilizuia jezi za RS Berkane zenye ramani ambayo mataifa hayo mawili yana mgogoro juu ya eneo ambalo linaonekana kwenye ramani hiyo.




Berkane wakagoma kuvaa jezi nyingine hivyo kupelekea mchezo huo usipigwe, baada ya kitendo hiko CAF ikawapa ushindi Berkane kwa sababu walinyimwa jezi na wenyeji.




Klabu ya USM Alger nayo ikasafiri hadi nchini Morocco ili kucheza mchezo wa marudiano cha ajabu leo ni kwamba hadi muda wa mchezo unafika USM Alger hawajaingiza timu uwanjani.




Hivyo sasa rasmi Fainali ya Kombe la Shirikisho baranin Afrika msimu huu itakuwa ni kati ya Zamalek SC ya Misri dhidi ya Berkane ya Morocco.

 

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post