Baada ya klabu ya Simba kutangaza kufikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na kocha Abdelhak Benchikha pamoja na wasaidizi wake wawili Kamal Boujnane na Farid Zemit.
Ameibuka Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally na kusema kuwa haikua rahisi Simba kumpata kocha kaliba ya Benchikha na hakuna aliyeamini kama wangeweza kumudu kuwa na kocha wa aina yake.
"Kumpata Mwalimu huyu ni ishara kuwa viongozi wetu walionesha dhamira ya dhati ya kuipeleka Simba kwenye kilele cha mafaniko makubwa zaidi. Ukubwa wa Mwalimu Benchikha na gharama za kuwa na Mwalimu wa aina yake ni dhahiri kuwa viongozi wetu wakiongozwa na Mo Dewji walijitoa mhanga kwa maslahi ya kuiboresha Simba yetu
"Juhudi ya kwanza ilikua ni kumleta Kocha jambo ambalo limefanyika kwa asilimia mia juhudi ya pili ilikua ni kubaki nae. Kocha kubaki kazini au Muajiriwa yeyote kubaki kazini hutegemea pia na matakwa ya muajiriwa binafsi"
"Wana Simba tutulie tuwape muda viongozi wetu watafute Kocha mwingine mzuri kwa maslahi ya timu, Kama waliweza kumleta Benchikha basi wanaweza kuleta yeyote mzuri kwa maslahi ya Simba yetu" amesema Ahmed Ally.

Kwa sasa kikosi cha timu hiyo kitakuwa chini ya Juma Mgunda hadi mwisho wa msimu, hata hivyo, Juma Mgunda atasaidiana na Selemani Matola kama Kocha Msaidizi,
.jpg)
Post a Comment