Ugomvi wa Mo Salah na Klopp uko hivi



Mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah alisema ikiwa atazungumza "kutakuwa na moto" baada ya kuzozana na kocha Jurgen Klopp kwenye mchezo wliotoka sare ya kufungana mabao 2-2 na West Ham.



Salah alionekana kugombana na Klopp wakati akijiandaa kuingia kama mchezaji wa akiba dakika ya 79.



Klopp alisema hatafichua mabishano hayo yalihusu nini, lakini mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Peter Crouch alisema kwenye TNT Sports kwamba "haionekani kuwa nzuri kwa kilabu".



"Salah ni mchezaji ambaye ameanza mechi nyingi kwa Liverpool na atakuwa na hasira kuwa kwenye benchi. Lakini hakuna anayependa kuona hili kati ya kocha na mchezaji muhimu."Crouch alisema.



Salah alionekana kuchanganyikiwa na jambo ambalo Klopp alimwambia na alionekana kutaka kurefusha ugomvi huo kabla ya wachezaji wenzake Darwin Nunez na Joe Gomez kumtuliza.





Katika video kwenye mitandao ya kijamii, Salah, alipokuwa akipitia eneo la vyombo vya habari baada ya mechi, alisema: "Nikizungumza kutakuwa na moto."




Mwandishi wa habari aliuliza "Moto?" na Salah akajibu: "Ndiyo, bila shaka."



Klopp alisema baadaye: "Tulizungumza juu ya hilo kwenye chumba cha kubadilishia nguo na imefanywa kwa ajili yangu."






Klopp ataondoka mwishoni mwa msimu huu na Liverpool wiki hii walikubali kulipa fidia ya hadi £9.4m katika klabu ya Feyenoord kwa ajili ya kupata saini ya kocha wa klabu hiyo Arne Slot.



Pia kumekuwa na uvumi kuhusu mustakabali wa Salah, ambaye amefunga mabao 210 katika mechi 346 katika kipindi cha miaka saba akiwa Liverpool lakini mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu ujao.



Alihusishwa na kuhamia katika Ligi Kuu ya Saudi Arabia msimu uliopita na tetesi hizo zimeanza kuenea kwa mara nyingine.



Mshambuliaji wa zamani wa Rangers, Ally McCoist aliiambia TNT Sports: "Amekuwa mmoja wa wachezaji bora ambao tumeona kwenye ligi hii hakuna kitu cha kushangaza kwa Liverpool lakini kiwango chake kimeshuka"




Salah amefunga mabao 24 katika mechi 41 akiwa na Liverpool katika mashindano yote msimu huu.



Beki wa zamani wa Liverpool Stephen Warnock aliiambia BBC Radio 5 Live kwamba mabishano hayo yalikuwa "mgongano wa majisifu. Uhusiano kati ya wawili hao unapaswa kuwa wa heshima, na kuheshimu jinsi wamesaidia kazi za kila mmoja"

 

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post