Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba Sc Abdelhak Benchikha ameripotiwa kuachana na klabu hiyo kwa makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba kwa muda uliosalia.
Benchikha alipewa nafasi hadi mwisho wa msimu ila ameuomba uongozi wa Simba kuondoka.
Kwa mujibu wa ripoti Benchikha ambaye alijiunga na Wekundu hao wa Msimbazi mnamo Novemba 27, 2023 baada ya kuachana na USM ALGER ya Algeria, akichukua mikoba ya Robertinho aliuomba uongozi wa Simba Sc kuondoka kabla ya mwisho wa msimu.
Ripoti zinadai kikosi cha Wekundu hao wa Msimbazi kitakuwa chini ya Kocha Juma Mgunda kwa muda akisaidiwa na Seleman Matola, huku Kocha Michael Igendia akisalia kuwa kocha wa viungo.

Post a Comment