Ajax wana nia ya kumteua meneja wa zamani wa Chelsea na Brighton Graham Potter, ambaye pia yuko kwenye orodha ya Manchester United ya watu wanaoweza kuchukua nafasi ya Erik ten Hag. Potter amekataa ofa ya kwanza kutoka kwa Ajax kwa sababu mshahara uliopendekezwa haukukidhi matarajio yake. (Chanzo : Guardian)
Meneja wa zamani wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer na mkufunzi wa zamani wa Leeds United Jesse Marsch wamewasiliana na Canada kuhusu kuiongoza timu ya taifa katika Kombe la Dunia la 2026. (Chanzo : Standard)
Klabu ya Bundesliga Stuttgart iko tayari kufanya uhamisho wa fowadi wa Ujerumani Deniz Undav, 27, kuwa wa kudumu baada ya kumsajili kwa mkopo kutoka Brighton msimu uliopita wa joto. (Chanzo : Caught Offside)
Manchester United itamlenga beki mpya wa kati, kiungo wa kati na mshambuliaji katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi, huku mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 28, akiwa miongoni mwa wachezaji ambao hawapo tena katika mipango ya klabu hiyo. (Chanzo : Football Insider)
Arsenal wanafuatilia wachezaji wengi wanaolengwa katika safu ya kati huku kukiwa na wasiwasi kwamba mkataba wa kiungo wa kati wa Real Sociedad na Uhispania Martin Zubimendi, 25, unaweza kuwa mgumu kufikiwa.( Chanzo : Standard)
Manchester United wana imani dau la kati ya £60-70m litatosha kumsajili beki wa Uingereza Jarrad Branthwaite, 21, kabla ya Juni 30, na hivyo kuiruhusu Everton kujumuisha ada hiyo katika akaunti zao za 2023-24 na kuepuka kukatwa pointi zaidi. (Chanzo : Football Insider)
Arsenal na Manchester City wamefahamishwa kuwa Newcastle United wako tayari kusikiliza ofa zinazozidi thamani ya £80m kwa kiungo wa kati wa Brazil Bruno Guimaraes, 26, msimu huu ujao. (Chanzo : 90min)
Manchester United wanaweza kuanza kusaka usajili wa beki wa kushoto wa Uhispania Miguel Gutierrez, 22, kutoka Girona lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Arsenal na West Ham. Kifungu cha kutolewa cha Guimaraes cha pauni milioni 100 kitaanza kutumika kwa mwezi mmoja pekee, kuanzia mwishoni mwa Mei hadi mwishoni mwa Juni.( Chanzo : Fabrizio Romano, Caught Offside)




Post a Comment