Simba SC Wafikia Rekodi ya Yanga Kombe la Muungano





Klabu ya Simba imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Muungano 2024 baada ya kuifunga klabu ya Azam FC bao 1-0.



Bao pekee la Babacar Sarr dakika ya 77' limetosha kuipa ushindi Simba SC katika mchezo wa Fainali ya Kombe la Muungano uliopigwa katika dimba la New Amaan Complex, Zanzibar.



Kihistoria Simba wametwaa Kombe la Muungano mara 6, sawa sawa na watani zao Yanga ambao nao wametwaa Kombe hilo mara 6.



Simba ilitinga Fainali baada ya April 24 kuichapa KVZ mabao 2-0 katika mchezo wa Nusu Fainali ya kwanza ya Mashindano hayo.



Azam FC nayo ilifata Simba baada ya kuichapa KMKM mabao 5-2 katika mchezo wa Nusu Fainali ya pili.



Michuano hiyo imerejea mwaka huu 2024 baada ya kukosekana kwa zaidi ya miaka 20 tangu iliposimama kufanyika.





 

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post