Ally Kamwe Atoa Neno Baada Simba Kutwaa Kombe la Muungano




Msemaji wa klabu ya Yanga 'Wananchi', Ally Kamwe ametoa pongeza kwa watani zake Simba SC baada ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Muungano 2024 visiwani Zanzibar.



Kamwe ameipongeza Simba SC kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kwa kuandika "Nichukue fursa hii kuwapongeza sana watani kwa kubeba Kombe la kubwa la Muungano.



"Haya ni mafanikio makubwa sana yaliyotokana na timu bora na viongozi imara mliokuwa nao. Msimu ujao na sisi Yanga SC tutapambana ili tushinde Kombe ili kubwa la kihistoria" alisema Kamwe.



Simba imetwaa ubingwa wa Kombe la Muungano baada ya kuifunga Azam FC bao 1-0 katika mchezo wa Fainali uliopigwa katika dimba la New Amaan Complex, Zanzibar.



Bao pekee na la ushindi katika mchezo huo lilifungwa na Babacar Sarr dakika ya 77' na kuifanya Simba kufikia rekodi ya Yanga SC ya kutwaa Kombe hilo mara 6.

 

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post