Timu ya mpira wa rede ya The Blue Nage Queens ya visiwani Zanzibari imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Bonanza la Nage Muungano Cup 2024 baada ya kuifunga timu ya Temeke Combine ya Dar es Salaam.
The Blue Nage Queens wametwaa ubingwa huo baada ya kuifunga timu ya Temeke Combine mabao 20-2, huku timu ya Msufini Quens kutoka Chamazi jimbo la Mbagala ikimaliza kuwa washindi wa tatu katika Bonanza hilo maalum la kusherekea Miaka 60 ya Muungano lilofanyika viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo kumalizika, Princess Nicodem ambayeni Afisa Habari wa Umoja wa timu za mchezo wa rede mstali kati wilaya ya Tememe amesema wamejifunza mchezo wa Nage na kutoa sababu za kupoteza mchezo huo.
"Kwanza nitoe pongezi kwa wote walioshiriki katika Bonanza ili binafsi nimefurahi sana kuona mchezo wa Nage, kwetu sisi Temeke leo hapa tumejifunza, maana sisi tunacheza mchezo wa rede mstali kati tofauti na wenzetu wancheza hii Nage"
"Mchezo huu wa Nage unavutia sana, japo kwetu sisi huu sio sana kucheza, lakini sasa tunahaja na sisi sasa kujifunza rede zote ya mstali kati na hii ya Nage ili siku nyingine wakija tuwape dozi" alisema Nicodem.
Kwa upande timu ya The Blue Nage Queens, baadhi ya viongozi wao wameonesha kufurahishwa na Bonaza hilo huku wakiwataka viongozi hao wa Temeke kuendelea kushirikiana na wakatumia nafasi hiyo kuwakaribisha Zanzibar.


Post a Comment