RASMI : Benchikha aondoka Simba SC




Klabu ya Simba imetangaza kufikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Abdelhak Benchikha pamoja na wasaidizi wake wawili Kamal Boujnane na Farid Zemit.



“Mwalimu Abdelhak Benchikha ameueleza uongozi wa Simba kuwa anauguliwa na mkewe, hivyo anahitaji muda kuwa karibu naye na kumuuguza” inaeleza taarifa ya klabu hiyo iliyotolewa leo.



Kwa mujibu wa taarifa ya timu hiyo kwa sasa kikosi hicho kitakuwa chini ya Kocha Juma Mgunda akisaidiwa na Selemani Matola mpaka Bodi ya Wakurugenzi itakapotoa uamuzi mwingine.






 

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post