Odegaard Nahodha wa ajabu ndani ya Arsenal




Uamuzi wa kocha Mikel Arteta wa kumtaja Martin Odegaard kuwa nahodha wa Arsenal Julai 2022 ulikabiliwa na shaka wakati huo, lakini imeonekana sasa kuwa ni uwamuzi bora sana.



Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ameongoza kwa mfano ndani na nje ya uwanja na anaweza kuwa nahodha wa kwanza wa Arsenal kunyanyua taji la Premier League tangu Patrick Vieira alipofanya hivyo mwaka 2004.



Tangu awasili katika klabu ya Arsenal akitokea Real Madrid Januari 2021, awali kwa mkopo, Odegaard amefanya makubwa kaskazini mwa London na ushawishi wake umekuwa ukiongezeka wakati huu The Gunners wakisaka ubingwa wa Ligi Kuu ya England.



Muongo mmoja uliopita, Arteta (ambaye kocha kwa sasa) alikuwa nahodha wa The Gunners kwa misimu miwili hadi alipostaafu mwaka 2016, na kumfanya kuwa mmoja wa majaji bora wa kumteua Odegaard jukumu hilo.




Raia huyo wa Norway alichukua nafasi hiyo kufuatia kuondoka kwa Pierre-Emerick Aubameyang na nahodha wa muda, Alexandre Lacazette.



Odegaard alipoteuliwa kuwa nahodha, Arteta alisema: "Nilichoona kwa miezi 18 iliyopita tangu amekuwa nasi, aliwakilisha maadili ya klabu hii ya soka, timu, wachezaji wenzake na wafanyakazi kwa njia bora zaidi. Pia ni nahodha wa timu yake ya taifa na nadhani ulikuwa wito sahihi, na ninajivunia kutangaza hivyo kwa sababu nadhani ni mtu mzuri sana"


Lakini ulikuwa uamuzi ambao ulikuja kama mshangao kwa baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo. "Nilishangazwa kidogo, kulingana na umri wake," alisema shabiki wa Arsenal, Pippa Monique.



Lakini sasa tumeona kuimarika kwa kiwango cha juu katika uchezaji wa timu, matokeo na ari kwa kuwa Odegaard amevaa kitambaa. Na iendelee kuimarika kwa muda mrefu. Odegaard amekuwa mfano mzuri kwa wachezaji wenzake msimu huu, huku mchezaji huyo akichangia mabao nane na asisti nane kwenye ligi kuu.



Mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway alikufunga penati ya kwanza katika mikwaju ya penati, wakati Arsenal ilipoichapa Porto na kutinga hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 14 mwezi uliopita.



"Napenda kupiga penati ya kwanza kwenye mikwaju ya penati, nadhani hiyo ni muhimu kwangu kufanya hivyo, na kujaribu kuhakikisha tunaanza vyema" Odegaard alisema





Odegaard alitawazwa kuwa mchezaji bora wa mechi katika sare ya 2-2 na Bayern Munich akitengeneza nafasi nyingi zaidi (tano), akipiga pasi nyingi zaidi (29) na usahihi wa pasi ulikuwa wa 88%.



Akizungumza kabla ya Arsenal kutoka sare dhidi ya Manchester City, fowadi wao chipukizi na raia mwenzake wa Odegaard, Oscar Bobb alisema: "Ni ndoto kucheza na Martin ni mmoja wa wachezaji bora zaidi namba 10 duniani"



Katika ushindi wa Arsenali wa mabao 2-0 dhidi ya Wolves, Odegaard alihitimisha ushindi huo kwa kufunga bao dakika za lala salama (90+5'). Kisha akafuatia kwa kiwango cha hali ya juu, akitoa pasi mbili nzuri za mabao Arsenal ilipowazaba wapinzani wa London Chelsea 5-0 huko Emirates siku ya Jumanne.



Odegaard alionyesha kujitolea kwake kwa The Gunners kwa kutia saini mkataba mpya Septemba 2023, ambao utamweka klabuni hapo kwa miaka mitano.



Arteta alipoulizwa ni kiasi gani Odegaard anaiendesha timu kama nahodha, alisema "Amepiga hatua kubwa. Uwepo wake, jinsi anavyojiendesha mbele ya wachezaji wenzake na viwango anavyoweka ni bora."



The Gunners watavaa na Tottenham kesho Jumapili, April 28, 2024.

 

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post