Leicester Warejea Premier League



Klabu ya Leicester City imepanda daraja kutoka Championship hadi Ligi Kuu ya England 'Premier League" baada ya klabu ya Leeds United kupokea kichapo kutoka kwa Queens Park Rangers.


Kichapo cha mabao 4-0 walichokipata Leeds United katika uwanja wa Loftus Road kinamaanisha vijana wa kocha Daniel Farke wanasalia nafasi ya pili ya Championship wakiwa na alama 90 tofauti ya alama nne na vinara Leicester wenye alama 94 wakiwa wamesalia na michezo miwili mkononi wakati Leeds United wakisaliwa na mchezo mmoja tu.


Leicester wanaweza kujikusanyia alama 100 kama watapata alama sita katika michezo yao miwili iliyosalia hukuwa wakiwa na uwakika wa kurejea ligi kuu baada ya kushuka daraja msimu uliopita.


Leicester wanaweza kunyakua taji la Championship siku ya Jumatatu, wakipata ushindi dhidi ya Preston ikiwa Ipswich inayoshika nafasi ya tatu itashindwa kuifunga Hull City leo Jumamosi.


Ipswich inaweza kujiunga na Leicester katika Ligi Kuu ya England 'Premier League" msimu ujao ikiwa itavuna alama tano katika mechi zao tatu zilizosalia.



Top 10 ya Championship




 

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post