Ancelotti Afurahia Xavi Kusalia Barcelona

                                                                                                                            



Kocha mkuu wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amesema kwamba chaguo la Xavi Hernández kusalia kama kocha wa Barcelona ni “uamuzi sahihi.”


Xavi, 44, alitangaza kwamba angeondoka kwenye wadhifa huo mwishoni mwa msimu huu, lakini sasa amechagua kusalia kuinoa klabu hiyo hadi mwisho wa mkataba wake mnamo 2025.


“Nadhani Xavi amefanya kazi nzuri (katika klabu ya) Barcelona. Anaijua klabu vizuri sana (aliwahi kucheza) kwangu kuamua kubaki ni uamuzi sahihi"


“Tunapaswa kuheshimu kwamba watu wanaweza kubadilisha maoni yao. Ni mara ngapi nimebadilisha maoni katika kazi yangu? Inaruhusiwa.” alisema Ancelotti.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post