Mwanaharakati kutoka Ghana, Abubakar Tahiru mwenye umri wa miaka 29 amefanya jaribio la kuvunja rekodi ya 'Guinness World Records' ya kukumbatia miti.
Tahiru amekumbatia jumla ya miti 1,123 kwa dakika 19 kila mti, jaribio lake lilifanyika katika Msitu wa Kitaifa wa Tuskegee, moja ya misitu minne ya kitaifa katika jimbo lenye utajiri wa mbao la Alabama, Marekani.
Tahiru amelelewa katika jamii ya wakulima huko Tepa, Ghana, ambako ni mwanaharakati wa asili na uhifadhi wa mazingira.
Mwanaharakati huyo anasema sehemu ngumu zaidi ya jaribio la rekodi ilikuwa ni kulazimika kusogea haraka kati ya miti huku akihakikisha kwamba kila kumbatio linakidhi viwango vinavyohitajika na 'Guinness World Records'.
Kwa madhumuni ya rekodi hii, kukumbatia kunafafanuliwa kama mikono yote miwili kuzungushiwa mti kwa karibu. Hakuna mti unaoweza kukumbatiwa zaidi ya mara moja, na hakuna uharibifu unaoweza kusababishwa kwenye mti wowote la sivyo jaribio litakataliwa.

.jpg)
Post a Comment