TEJA YAPIGA 'STOP' VILABU VYA JOGGING TEMEKE KUSHIRIKI BONANZA LA WASAFI JOGGING



 

Chama cha Jogging wilaya ya Temeke (TEJA) kimepiga marufuku vilabu vya Jogging katika wilaya hiyo kushiriki katika Bonanza la Wasafi Jogging Promotion linalotarajiwa kufanyika Januari 19, 2025 katika fukwe za Coco Beach Jijini Dar es Salaam.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Mwenyekiti wa TEJA, Rashid Pazzi, Januari 12, 2025 imesema "Siku za karibuni kumekuwa na sintofahamu kwa wana Temeke kwenye kushiriki Bonanza  linaloandaliwa na Wasafi FM Jogging Promotion tarehe 19/01/2025.


"Kamati tendaji iliamua kutoshirikiana na Club hiyo kutokana na sababu nyingi wakati  chama kikilinda hadhi ya chama na wanachama wake (Vilabu) kwa kutumiwa ama kudharauliwa na kutolewa kejeli zilizotoka kwa viongozi wa Klabu tajwa.




Tofauti hizi zilianza baada ya Wasafi FM Jogging Promotion kualika viongozi wa vilabu  vya Temeke bila kuomba idhini wala kutoa taarifa kwa TEJA, baadae katika Uzinduzi wa 
kuitangaza NBC Marathoni uliofanyika Leaders Club, walileta barua kutoka KIJA, lakini TEJA walitaka kujua vilabu vyake vitanufaika na nini kwa kuwa hiyo ni biashara na ni ya Media, nasi hatutoruhusu vilabu vyetu vitumike bila kupata faida yoyote. 


"Viongozi wa TEJA walipata maneno mengi ya kejeli na dharau (Yasioandikika hapa) kutoka Klabu tajwa na kusema wao wanaweza kufanya bila Temeke na litafana tu, jambo lilifanyika japo ushiriki 
wa Temeke ulikuwa finyu kabisa. 


"Yakaandikwa mengi kwenye mitandao tuliyapuuza. Wakaandaa jambo lingine likianzia Uwanja wa Karume mpaka Viwanja vya Gwambina,  mara hii hatukupata barua yoyote na wala hawakuombwa kibali cha kufanya bonanza hilo kwenye eneo letu la Temeke, na hawaku mtaarifu Afisa michezo wa Wilaya ili kupata kibali, mara hii tena wanatemeke hawakushiriki kabisa. 


"Yalisemwa mengi sana kwenye mitandao ni kwamba hawatoshirikiana na Temeke katika jambo lolote, na wakatekeleza  hayo kwa vitendo kwa kutoshiriki Bonanza la TEJA la 2023 na 2024 huku wakitangaza kwenye media zao kuwa hakuna jambo la jogging katika wiki ya Bonanza letu na wakisema  kuna Marathoni au jambo lingine ambalo wao walienda kulifanya.




"Uongozi wa TEJA ukatathimini hayo na kuamua nasi wana Temeke hatutashirikiana nao pia, na ndio maana mabonanza yote hatukutaka kutumia Media ili kujikinga na dharau na  kejeli, lakini mnamo Januari 05 /2025 kupitia chama chao cha wilaya (KIJA) waliomba tukutanishwe nao ili kuondoa sintofahamu hizi. 



"Tulifanikiwa kukutana na Viongozi wa TEJA,  KIJA na wa Club hiyo kwenye eneo la Michelle’s Pub, baada ya majadiliano marefu na wao kukubali makosa yote na kuomba msamaha wa maneno, tukafikia muafaka kwa masharti 
yafuatayo;



1. Wasafi FM Jogging Promotion waandike barua ya kuwaomba msamaha wana  Temeke na kukili makosa yao yote.

2. Barua lazima ipitie kwa chama chao (KIJA) kwa kuwa TEJA hatupaswi kuwasiliana 
na Klabu ya wilaya nyingine moja kwa moja sababu si mwanachama wetu


3. Baada ya kupokelewa kamati tendaji itakaa na kuwapa majibu ya hayo maombi ya msamaha na kuruhusu vilabu kushiriki Bonanza hilo.


Kwa masikitiko makubwa kabisa yale tuliyokubaliana kwenye kikao cha usuluhishi hayakutekelezwa kikamilifu, Waliandika barua na kututumia siku Jumanne tarehe 7/1/2025 bila kuielekeza 
kwenye chama chetu.


Barua waliituma moja kwa moja kwetu bila kupitia kwenye chama chao (KIJA), kwa maana haikuwa na anuani ya KIJA wala muhuri pia Saini ya Katibu wa chama haikuwepo.



"Licha kuwasiliana na viongozi wa Chama KIJA na Wasafi FM Jogging Promotion kuirekebisha barua na kuituma tena hakuana kilichotekelezeka, tumekuwa tukipewa ahadi tu, Mpaka siku ya Jumapili tarehe 12/01/2025 hatujapokea barua yao kama 
tulivyokubaliana na walivyoahidi.


"Bado waliendelea kuwapigia Vilabu vyetu kabla ya kutuma barua ama nasi kuwaruhusu. Na wameendelea kusambaza taarifa za uongo zenye nia ovu ya kwamba, washaleta barua kwetu na ila TEJA ndio hatutaki kuwajibu na tuna ajenda zetu. Wanaamishia tuhuma na kusema kuwa sababu sio barua bali kuna ugomvi kati ya Mtu na Mtu ndio maana tunazuia vilabu.







 

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post