MADRID YAPATA PIGO KUELEKEA MECHI DHIDI YA LIVERPOOL



Klabu ya Real Madrid imesema itamkosa mshambuliaji wake Mbrazil Vinicius Jr katika mchezo wao wa UCL ugenini dhidi ya Liverpool baada ya kupata jeraha la misuli ya paja licha ya kucheza mechi nzima katika ushindi wa 3-0 La Liga walioupata jana dhidi ya Leganes.


Madrid ambao wapo katika nafasi ya 18 kati ya timu 36 katika msimamo wa Ligi ya mabingwa watasafiri hadi Anfield Jumatano kumenyana na Liverpool walio kileleni mwa msimamo huo.


Kwa mujibu wamagazeti ya nchini Uhispania Vini atakuwa nje kwa muda wa wiki 3 na atarejea kwenye fainali ya Kombe la Mabara mjini Doha, Disemba 18, 2024.


Kwa upande wa Liverpool huenda wakamkosa Trent Alexander-Arnold dhidi ya mabingwa hao mara 15 wa UCL baada ya kumkosa katika ushindi wa jana 3-2dhidi ya Southampton kutokana na jeraha la misuli ya paja alilolipata kabla ya mapumziko ya mechi za kimataifa.



 

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post