Mchambuzi maarufu wa Soko Nchini Jemedari Said amesema Kocha kutoka Algeria KHEIREDDINE MADOUI anatajwa kuwa mrithi wa Miguel Gamondi kwenye klabu ya Yanga.
Gamondi anatajwa kuondoshwa kutokana vitu vingi ikiwepo mwenendo mbaya wa Yanga kwenye mechi mbili za mwisho za Ligi Kuu ya NBC.
"Jeuri, kiburi, kutoshaurika, ubishi, kupoteza ushawishi kwenye timu na wachezaji (dressing room) kutoelewana na wasaidizi wake vinatajwa kuwa vitu vinavyomuondoa Gamondi Yanga"
"Inasemekana mpaka sana Gamondi ana elewana na msaidizi wake mmoja tu ambaye ni Msenegal MOUSSA NDAW lakini wengine haelewani nao" amesema Jemedari
Taarifa zinasema Moussa Ndaw huenda naye akaondoka na bosi wake Gamondi ili kupisha utawala mpya.
Pia kuna habari, Gamondi na kocha wa makipa kurushiana maneno makali katika hoja ya kutoelewana na wasaidizi wake.

Post a Comment