Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti amesema anauhakika kuwa mchezaji wake Vinicius Jr atashinda tuzo ya Ballon d’Or zitakazotolewa Jumatatu ya Oktoba 28 huko Paris Ufaransa.
Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 24 alifunga hat-trick ya kuvutia dhidi ya Borussia Dortmund kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa uliopigwa jana na kusaidia timu yake iliyokuwa nyuma kwa magoli 2-0 na kushinda 5-2 Santiago Bernabeu.
Mashabiki wa Real Madrid waliliimba jina Vinicius Jr kuwa atashinda tuzo hiyo kubwa ulimwenguni na baada ya mechi Carlo Ancelotti alimwita Vinicius Jr na kusisitiza kuwa atashinda Ballon d'Or kutokana na ubora aliouonesha msimu uliopita.
Kwa upande wake mshambuliaji huyo wa Brazil alipoulizwa kuhusu kushinda tuzo hiyo alijibu kwamba malengo yake ni kusalia Real Madrid na kuendelea kuweka historia ndani ya klabu hiyo mabingwa mara 15 wa UCL.

Post a Comment