Ukurasa wa EFM Jogging Club kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram umetoa taarifa ya kurejea kwa waimbaji wao wawili, MC Dumayo na MC Fagio ambao walikuwa katika kikundi cha Wasafi Jogging.
Katika taarifa ya EFM Jogging Club, ilisema sauti za vijana hao, wenye uwezo mkubwa wa kuimba zimekuwa chachu kubwa kwa watu wengi wanapokuwa katika mbio zao za pole.
"Hii ndio nyumba ambayo vijana hawa walikuzwa na kulelewa kwa upendo na amani. Haijawahi kuwa rahisi kwao kuishi ugenini bila kukumbuka nyumbani.
Tuliwafundisha maadili wakaenda kuwafundisha na kuelimisha wengine. Sasa wamerejea kundini kuendelea kuibeba Club namba moja Ulimwenguni, Efm Jogging Club.
Sauti zao zimekuwa zikipenya masikioni kwa kila mtu wa mazoezi. Burudani zinazosindikia kilometres nyingi ambazo ndio pumzi ya wakimbiaji.
Taarifa hiyo imeendelea kwa kuwamwagia sifa vijana hao kuwa ni waimbaji ambao wameteka soko kwa sasa.
Kwa mara ya kwanza wameonekana wikiendi iliyopita katika Bonanza la Clouds Jogging lililofanyika Msasani Club.
Vijana sasa wanaungana na MC Mwenga Mwanzo kuongeza ubora katika club hiyo yenye masikani yake Coco Beach, Dar es Salaam.
PICHA ZAIDI


.jpeg)

Post a Comment