Shirikisho la mpira wa miguu nchini Uholanzi (KVNB) limemfungia maisha kujihusisha na soka mwamuzi Jan Smit kufuatia maamuzi mabovu na yasiyoridhisha aliyoyafanya kwenye mchezo wa Ligi daraja la nne kati ya Saint George dhidi De Valken.
Mwamuzi huyo mwenye umri wa miaka 61 alitoa kadi nyekundu tatu, kadi zote zikienda kwa timu ya De Valken (wachezaji pamoja na kocha wao)
Baada ya dakika 90 kukamilika wakati mchezo huo ukiwa sare ya kufungana mabao 2-2 aliamuru ziongezwe dakika 15 za nyongeza

Katika dakika 15 hizo za nyongeza golikipa wa klabu ya St George alifunga bao na kupelekea Mchezo huo kutamatika kwa mabao 3-2
Baada ya mchezo, mwamuzi Smit alijiunga, kusheherekea na timu ya St. George, kwa kuimba na kushikilia kombe la ubingwa
Kitendo hicho kiliwachukiza viongozi wa timu ya De Valken na kuamu kuwasilisha malalamiko, na KNVB kuchukua hatua ya kumfungia mwamuzi huyo
Smit mwenyewe hakubaliani na uamuzi huo alisema baada ya kufungiwa "Niliimba tu wimbo na kuinua kombe mara moja. Hilo ndilo jambo pekee. Ninaona huzuni sana".

Post a Comment