YANGA WANA CHANGAMOTO SOKA LA VIJANA NA WANAWAKE



Kuna ukweli mmoja huwa hausemwi ila tunapaswa kuusema haswa kuhusu YANGA, wana changamoto kubwa sana kwenye SOKA LA VIJANA na SOKA LA WANAWAKE, timu yao imestuck kabisaa haipigi hatua, haiendi mbele na hairudi nyuma ipo tu pale kati imestuck, katika dunia ambayo soka la Wanawake na Vijana linapiga hatua wao wapo pale pale.



Simba inaweza kuwa na matatizo mengi sana ila kuhusu mipango haswa kwa soka la Wanawake hilo sio tatizo lao, hapa kati waliyumba kidogo kuhusu soka la Vijana baada ya kupiga kelele haswa masuala ya posho kwa Vijana naona timu ikatulia na sasa imefuzu hatua ya mtoano UNDER 20 na UNDER 17 wanafanya vizuri tu kwenye project yao.






Lazima tuulizane au tuweke vitu open, timu za Wanawake na Vijana kwa Yanga zipo serious kweli au kukidhi matakwa ya CLUB LICENSE? Hapo ni lazima tuchore mstari na sauti ipazwe, suala sio kusajili tu bali kwa mipango ipi na mfumo upi? Mna changamoto zipi na utatuzi upo vipi?




Kumwona Simba na JKT QUEENS kimataifa iwe chachu kwenu Wananchi, Simba wamewageuza Wateja wanajipiga nje ndani, wanawafanya watakavyo, jibu ni jepesi tu UWEKEZAJI, Simba kawekeza sana soka la Wanawake na kuna hela tena nyingi tu, ni rahisi mno kuleta ubingwa wa Afrika kwa Wanawake kuliko nusu fainali Klabu bingwa kwa Wanaume.






WANANCHI wekezeni kweli, kuweni na mipango haswa ya soka la VIJANA NA WANAWAKE, mmeachwa mbali saaaaaana! Soka la Vijana hampo hatua ya mtoano na soka la Wanawake hampo kwenye mbio za ubingwa hata, ni mbio za Simba na JKT.



Ameandika Mchambuzi wa Soka, Farhan Kihamu, katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamiii wa X zamani Twitter.



 

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post