RAIS SAMIA AIONYA SIMBA FAINALI YA KOMBE LA MUUNGANO

 




Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameitahadharisha klabu ya Simba kuto kuwadharau Azam FC kuelekea Fainali ya Muungano Cup ambayo itapigwa hapo kesho.


Akizungumza leo Aprili 26, 2024 kwenye kilele cha miaka 60 ya Muungano, Rais Samia amesema Simba haitakiwi kuidharau klabu ya Azam FC kwenye mechi ya Fainali itakayochezwa kesho Jumamosi, Saa 2:15 Usiku kwenye uwanja wa New Amaan, Zanzibar.

"Nina washukuru waandaaji wa mashindano mbalimbali ikiwemo Ligi ya Mpira wa miguu ya Muungano, ambayo timu ya mdogo wangu Kassim (Majaliwa, Waziri Mkuu) imeingia kwenye fainali hizi za Muungano lakini wasiwadharau sana Azam huenda matokeo yakawa mengine kabisa" alisema


Michuano ya Muungano imerejea mwaka huu baada ya kukosekana kwa muda mrefu (miaka 20) tangu iliposimama kufanyika.


Ligi ya Muungano ilianza rasmi mwaka 1982 lengo ni kudumisha Muungano wetu na kutoa usawa wa kiuwakilishi katika michuano ya kimataifa ya vilabu, hii ni kutokana na Tanzania bara kuwa na ligi yake na Zanzibar kuwa na ligi yake

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post